You may have to Search all our reviewed books and magazines, click the sign up button below to create a free account.
Nasema Kiswahili is a friendly guide that helps anyone interested to learn Kiswahili. This book is not like others because it makes you feel comfortable while reading it. It also has some questions in every chapter and also it has the answers at the back which helps you to practice by yourself. I can promise you that within a week you will have mastery of Kiswahili language via this manual.
Kiswahili language is among the easiest language to learn over the world's languages. This is due the fact that, you pronounce a word as you write it. This is contrary to Indo-European languages such as German, English and French to mention just a few whose pronunciations are quite different from how they are written.
Nasema Kiswahili “I speak Swahili”, is a fully integrated Kiswahili language learning manual from the Beginner level to the Intermediate and the Advanced levels. The grammar of the language is well and clearly described. Each chapter is enriched with exercises and practice sections. The book will be very useful to Kiswahili learners at home and, more specifically, to learners in Kenya and Tanzania that need a full course in a single and clear book. The e-book version will also be helpful for moving people, expats, travellers, business(wo)men, tourists and students.
Msukumo wa kukiandika kitabu hiki ulikuja baada ya kupangiwa nifundishe kozi hii ya wageni. Hii ni kozi kwa ajili ya wanafunzi wageni ambao Kiswahili siyo lugha yao mama. Wanafunzi hawa wanataka kukuza stadi zao za uandishi, mazungumzo, usomaji na usikivu. Kwa hiyo, Idara yangu ikaona ni vema kunipangia nifundishe kozi ya misingi ya utungaji kwa wanafunzi wageni KF 300, kutokana na uzoefu wangu mdogo nilionao katika kufundisha wageni Kiswahili na kufundisha wazawa kozi za uandishi na ubunifu. Nilijiandaa vilivyo ikiwamo uandikaji wa kitabu hiki ili kinisaidie mimi binafsi kufundisha vizuri lakini pia kimsaidie mwanafunzi anayesoma kozi hii.Kitabu kimeandikwa kwa kuzingatia uzoefu na tajiriba anayokuwa nayo mwanafunzi mgeni kwa hiyo hata mazoezi yake ni mepesi mno (kwa mzawa) lakini ni magumu kwa mgeni. Kwa hiyo, mwanafunzi mgeni afundishwe kwa kutiwa moyo badala ya kuvunjwa moyo, kwa sababu kujifunza lugha ya kigeni siyo jambo jepesi.
Mashindano ya BSS na TPF yalifanyika nchini Tanzania mwaka kwa ajili ya kuibua vipaji vya wasanii chipukizi. Kutokana na mwenendo wa uteuzi wa washindi wa shindano hilo, mwandishi wa kitabu hiki alivutiwa kufanya utafiti na kutoa mapendekezo yake ya namna bora ya kuwapata washindi ambao ni wasanii. Soma kitabu hiki ili ufahamu mapendekezo hayo.
Filamu ni fasihi. Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya filamu na fasihi. Uhusiano huo unatokana na ukamilishanaji wa pande zote mbili kama anavyoelezea Perrier (1992) kwamba, fasihi inatoa mwangaza kuhusu filamu, na filamu inathibitisha thamani ya fasihi. Mtaalamu mwingine ambaye anaonesha uhusiano huo ni Jann (2001) anayeelezea kuwa, filamu kama ilivyo drama na tanzu simulizi kama vile riwaya, zote zinatumia usimulizi ili kufikisha ujumbe kwa hadhira. Hii ina maana kuwa, fasihi (tukichukulia mfano wa riwaya) ina mambo yanayoingiliana na filamu.Kazi zote zinatumia wahusika, msimulizi, ploti, lugha na mtazamo ili kusimulia hadithi. Katika riwaya, mwandishi anatumia sura wakati kwenye filamu anatumia fremu. Hadhira ya kiriwaya inatumia macho kusoma hadithi, wakati hadhira ya kifilamu inatumia macho kutazama filamu. Kwa hiyo, kuna mwingiliano kati ya fasihi na filamu.
Kitabu hiki cha muziki wa zamani wa Tanzania na harakati za ukombozi kinagusia baadhi ya nyimbo ambazo kwa 'namna' Fulani zinagusia suala la ukombozi. Ukombozi ni mada pana sana na jambo hili litajidhihirisha katika kitabu hiki.
Kitabu hiki kinahusu Sanaa ya uigizaji na misingi yake. Ni kitabu kinachomfaa mtu yeyote yule awe mkubwa au mdogo ambaye anapenda kujiongezea weledi katika Sanaa hii. Kitabu kinaelekeza namna ya kuigiza katika filamu, televisheni, redioni na jukwaani. Ni maarifa ambayo unaweza kuyapata kitabuni humu na ukaokoa fedha yako ambayo ingepotea kutokana na kuigiza kwa viwango 'duni' - jambo linalomaanisha kulipwa ujira mdogo. Lakini ukishajua namna ya kuigiza kwa misingi ambayo imedadavuliwa humu ndani, utaweza kukikuza kipato chako kwa sababu Sanaa yako itakuwa ya kiwango cha juu - na dau lako litakuwa juu (malipo yataongezeka kiwango kwa kuwa utakuwa mahiri katika Sanaa hii ya kuigiza - thamani yako itapanda).
Kitabu hiki kinahusu uchapishaji na uchapaji kwa lugha ya Kiswahili. Maarifa ya kitabu hiki yametokana na sababu mbalimbali ikiwamo kujisomea vijitabu mbalimbali, kufanya utafiti wa uwandani pamoja na uzoefu wangu mwenyewe katika sekta hii ya uchapishaji. Nilianza kufuatilia uchapishaji tangu nikiwa kidato cha sita, lakini sikufanikiwa kutokana na wachapishaji wengi kutaka fedha ndipo wachape kitabu. Lakini Mungu ni mkubwa kwani aliweza kufungua njia mbadala ya uchapishaji wa kisasa e-publishing ambao hauhitaji kutumia mbinu za kizamani katika mchakato wa uchapishaji na uchapaji. Kitabu hiki kimeandikwa kwa lugha inayoeleweka kwa msomaji wa kawaida ambaye anapenda kupata maarifa haya.
Kitabu hiki cha kiongozi cha mwalimu, kimekusudia kuwa mwongozo kwa ajili ya kuwafundisha wageni. Kitabu kinamwelekeza mwalimu namna ya kumfundisha mwanafunzi wa kiwango cha kwanza, cha pili, na cha tatu. Katika kila hatua ya kumfundisha mwanafunzi lugha ya Kiswahili, kumetumika mbinu mahsusi ili kuhakikisha mwanafunzi anafunzwa kwa umahiri mkubwa na anapata stadi ya kimawasiliano ya lugha ya Kiswahili. Kitabu hiki ni muhimu kwa mtu yeyote anayetaka kufundisha lugha ya Kiswahili kwa wageni.